THE INSTITUTE OF FINANCE
MANAGEMENT
IFM ALUMNI COMMUNITY
VIONGOZI CHUO CHA USIMAMIZI WA FEDHA WAPEWA MAFUNZO YA MAADILI KAZINI
Ofisi ya Rais – Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma (OR-SMVU), 24 Juni 2025, imeendesha mafunzo kwa Menejimenti ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha, ikijumuisha Wakuu wa Idara na Vitengo, Wativa na Wakurugenzi. Hizi ni juhudi za kuhakikisha viongozi hawa wanazingatia maadili ya umma na kufuata taratibu na kanuni za utumishi wa umma kama inavyoelekezwa na Serikali.
Mafunzo hayo yamefanyika katika Chuo cha Usimamizi wa Fedha, Kampasi ya Dar es Salaam, kwa njia ya ana kwa ana, na huku Kampasi nyingine wakifuatilia kwa kupitia TEHAMA. Mafunzo yaliendeshwa na Bi Magreth Vulla, akisaidiana na Bw. Saidi Katani na Bi Grace Matunda; maafisa Uchunguzi Waandamizi – OR-SMVU.
Katika mafunzo hayo, Afisa Vulla alisisitiza umuhimu wa viongozi kuwa na uadilifu wa kiwango cha juu, na kuzingatia sheria, taratibu na kanuni za utumishi wa umma. Alisisitiza kuwa maadili yanasaidia kutekeleza majukumu kwa lugha ya kusitirika, na yanawezesha mtumishi kujipima na kupima utendaji na matokeo ya kazi anazofanya.
Naye Bw Katani alielezea umuhimu wa kuweka Ahadi ya Uadilifu kwa Viongozi wa Umma, ili kukuza uwazi, uadilifu na uwajibikaji. Baada ya mafunzo ya Bw Katani, viongozi wa Chuo, ambao walikuwa hawajaweka ahadi hiyo, waliongozwa na maafisa hao na wakatoa ahadi yao ya uadilifu katika kutekeleza majukumu yao.
Naye Mkuu wa Chuo, akiwakilishwa na Dkt Herman Mandari, alisisitiza viongozi kufuata kwa umakini mafunzo hayo, na kuhakikisha yanatekelezwa kwa vitendo.
Mafunzo hayo ni sehemu ya juhudi endelevu za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Lengo ni kuhakikisha inaimarisha maadili katika utendaji wa viongozi wa umma na kuhakikisha ufanisi katika utoaji wa huduma kwa jamii ya Tanzania.
RELATED NEWS
- IFM ranks first among more than 50 Higher Learning Institutions (HLIs) in Tanz...
.
.
IFM conducted a public lecture with the theme “From Campus to Cashflow: Th...
The Institute of Finance Management (IFM) 4th Intake CFEs' graduation, organised...
IFM trained 26 Stanbic Bank staff who graduated as Certified Financial Educators...
P.O Box 3918, 5 Shaaban Robert Street
11101 Dar es salaam
+255 22 2112931-4
Fax : +255 22 2112935
alumni@ifm.ac.tz | +255222112931-4