THE INSTITUTE OF FINANCE
MANAGEMENT
IFM ALUMNI COMMUNITY
"CHARITY DAY 2025" WANAFUNZI WA KAMPASI KUU (DAR ES SALAAM)
Tarehe 27 Aprili 2025, Wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha walitembelea kituo cha kulea watoto cha Kisarawe Orphanage Home.
Watoto 53 wanaolelewa katika kituo hicho, ni wale waliotoka katika mazingira hatarishi.
Mahitaji yaliyopelekwa kituoni hapo ni vifaa vya shule, taulo za kike, vyakula, na pesa taslimu. Wanafunzi wa IFM waliambatana na walezi wao kutoka ofisi ya Huduma za Wanafunzi.
Shughuli hii ni mwendelezo wa utamaduni waliojijengea wanafunzi wa IFM, wa kutoa kwa jamii kila mwaka.
Wanafunzi wetu wanajifunza, wanahudumia, wanajijengea sifa na uzoefu, na wanashirikiana na jamii. Jambo hili huwapa sifa za kufanya vizuri kwenye soko la ajira na kujijengea sifa zinazohitajika na jamii, wafadhili, na ufadhili kwa ajili kuendelea na elimu ya juu.
TupoJuu#PopoteUtakapokwendaIFMniIleile#Daresalaam#Mwanza#Dodoma#Simiyu#Geita#Zanzibar#
RELATED NEWS
.
.
.
.
.
.
P.O Box 3918, 5 Shaaban Robert Street
11101 Dar es salaam
+255 22 2112931-4
Fax : +255 22 2112935
alumni@ifm.ac.tz | +255222112931-4